Thursday, June 20, 2013

Jinsi ya kuondoa Window Moja kwenye Pc yenye Windows Mbili

umeinstall window na ukashindwa kuiondoa ile ya zamani na kila ukiwasaha kompyuta inatokea hivi
AU HIVI
twende pamoja ili ujue njia rahisi ya kuiondoa window moja ambayo huiitaji JINSI YA KUIONDOA HIYO AMBAYO HUIITAJI 1. Bofya kitufe cha windows pamoja na R (Win+R) au fungua start menu kisha bofya "Run" 2. itafunguka dialog box ya run, andika neno "msconfig" bila "" kisha bofya ok 3. itafunguka dialog box "system configuration utility" kama unatumia windows xp chagua "boot.ini"kama unatumia later versions chagua kama hivi hapa chini.
4. chagua window ambayo huitaki kisha delete, baada ya hapo apply, na click ok 5. kompyuta itaakuuliza kama unataka kurestart au lah, finally, nenda kwenye folder lilikuwa na windows ya zamani (uliyoifuta)... mfano D:/windows.old (mwenyewe utakuwa unajua lilipo) kisha delete hilo folda. baada ya hapo restart pc yako na itakuwa ina window moja tu Kama umejifunza jambo jipya, au imekusaidia kiaina, bofya SHARE #sayay theComputerGUY

Download Adobe flash player (offline Installer) BUREEEEEEEEEEEEE!!!!!!!

IWAPO ULIKUA UNAANGALIA VIDEOz NYING KTK PC YAKO KWA KUKWAMAKWAMA (SCRATCHING) BASI BASI TATZO LAKO KWISHA KUANZIA LEO
jaman kwa wale wote waliokua na matatzo ya adobe flash player katka computer zao leo tatzo lao limekwisha chukua HAPA bure kabsa

Bomu Arusha Mkutano ChademA 15 JUNE

Wednesday, June 19, 2013

How to Install any font into any Computer Program

Windows phone vs Android

ni kawaida sasa hivi kwenye redio kusikia matangazo ya lumia, samsung galaxies zinazidi kushika kasi, techno wanakomba soko la tanzania na huawei nyingi za tigo zinazidi kusambaa. yote haya yanaweza kukuchanganya na kufanya usifanye uamuzi sahihi wakati wa kuchagua simu. hebu tuangalie windows phone ni nini na android ni nini na baadae utajua ufanyeje kuchagua simu sahihi. windows phone 8 hii ni operating system iliyotengenezwa na microsoft inatumika kwenye simu za nokia, htc, samsung na huawei mpaka sasa. imekuja kumreplace windows phone 7 ambayo haikupokelewa vizuri na wateja. tofauti na android windows phone inatumia tiles badala ya icon design yake hii imeipa umaarufu sana
Android hii ni operating system iliyotengenezwa na google na inatumika na watengeneza simu zaidi ya 80 wachache wao ni samsung, htc, huawei, tecno, sony, lg na asus. hii inatumia icon tofauti na windows phone. pia ina homescreen ambayo unaweza kueka app zako unazozipenda.
je ukitaka kununua simu ya windows phone uangalie nini? its about people vs apps kitu kimoja kizuri kuhusu windows phone ni uwezo wake wa kukusanya watu wote unaowajua na kuwaweka pamoja na kukupa habari zao zote. kuna peoples hub ambayo inakua na list ya marafiki zako na kama wana acount za facebook, twitter, unaona habari zote kwenye contact bila hata kufungua app ya twitter au facebook. ukitoa peoples hub kuna feature kama kids corner ambayo ni simu ya mtoto ndani ya simu yako, hapa unachagua application, video, miziki ambayo unataka mtoto wako aone akishika simu ili kumzua asifanye vitu vibaya. pia kuna rooms ambayo inakua ni private area kati yako na watu unaowapenda kama mke wako na wakwe zako eneo ambalo mtashare location na kila kitu. haya na mambo mengi yanaifanya windows phone kua very strong kwenye upande wa watu. one thing cool about android ni ina application nyingi sana. so far kuna application zaidi ya 700,000 wakati windows phone ina application 150,000 tu. hili linafanya vichwa vikubwa kama instagram kupatikana android na kukosekana kwenye windows phone.
so wakati unachagua simu uangalie mahitaji yako kati ya hivyo vitu viwili hapo juu. its about microsoft vs google kuna msemo siku hizi kuwa hununui simu bali unanunua ecosystem. huu msemo ni sahihi kabisa kwani kila platform siku hizi ina apps zake ambazo ni exclusive kwao tu, hapa nitaelezea ecosystem inayopatikana kwenye android na windows phone. kupunguza ukubwa wa thread nitazimention tu kama utataka maelezo zaidi utacoment microsoft office(wp) vs quickoffice(android) search (bing search) vs search (google search) map (nokia,bing map) vs map (google map) video (hakuna) vs video (youtube) mail (outlook,hotmail) vs mail(gmail) cloud(skydrive) vs cloud (google drive) video chat(skype) vs video chat (hangout) gaming (xbox) vs gaming (hakuna) hizi ni chache za muhimu so utaangalia ecosystem ipi unaipenda hapa nimeexclude apps za nokia maana ni special case. its about design vs customization kama nilivoelezea hapo juu windows phone imekuja na design mpya kabisa ya tiles ambazo ni live zinakupa information papo kwa hapo hizi tiles huwezi kuzichange na kuweka customization kama android lakini unaweza eka design unayotaka. unaweza resize tiles zikawa kubwa, za kati au ndogo na pia unaweza ukachange skin.
andoid yenyewe ipo vizuri kwenye customization kuliko windows phone unaweza ukaieka home screen yako the way unavyopenda wewe. zipo launcher mbali mbali zenye themes tofauti tofauti kwa kazi hii. kwenye android pia kuna launcher ambazo zinakuwezesha kuweka themes za 3d ili kuwezesha wewe kufeel tofauti ukitumia simu
its about security vs freedom kwenye windows phone mpaka sasa huwezi kuroot simu wala kufanya hacking ya aina yoyote simu imefungwa kila kona hili linaongeza ulinzi kwenye simu yako hutaathiriwa na virusi wala malware wa aina yoyote device itakua salama lakini tatizo linakuja unakosa uhuru hutaweza kufanya vitu unavyotaka wewe. kwenye android unakua huru unaroot simu unaeka custom firmware unafanya vitu unavyotaka wewe lakini tatizo linakuja kwenye security android kuna malwares wengi wanaweza wasiwe virusi lakini vitu kama spyware na adware ni vigumu kuviepuka kwenye android. its about productivity vs playing nafkiri hapa ndo pa muhimu zaidi panapozitenganisha hizi simu. kuwepo kwa microsoft office, skydrive, photobeamer, security kubwa, offline navigation na simu kuwa fasta kunaifanya windows phone kuwa nzuri kwa wafanya biashara kuliko android. kuwepo kwa HD games, na application mbali mbali kunaifanya android iwe simu nzuri ya kuchezea so hapa unatakiwa uangalie unahitaji nini je wewe unapenda kuchezea simu au unataka simu yako iwe productive? maana unaweza ukaenda windows phone then ukakuta games chache ukaanza kulalamika. na unaweza kuwa mfanya biashara ukaenda android ukaanza kulalamika betry na simu kuwa slow. pia kuhusu windows phone nimeongelea windows phone 8 na sio 7 better unaponunua simu ya windows phone ununue 8, kama huna uhakika ni vizuri uulize. #shukran sana kwa mshikaji wangu wa nguvu Chief-mkwawa #sayay theComputerGUY

Twitter Facebook

 
Powered by Blogger